Thamani yako iko katika kitu gani?
thamani ya maisha ya mwanaadamu ni matendo yake na sio umri wake. kuna watu wameishi maisha marefu sana katika dunia hii lkn thamani yao haionekani, lakini pia kuna watu wameishi maisha mafupi lakini mpaka sasa Dunia inawatambua, hii yote si kwa sababu ya wingi au uchache wa maisha waliyoishi bali ni kitu gani walifanya katika hayo maisha waliyoishi ndicho bado kinaishi katika jamii. usijiulize wala kujisifia wingi wa miaka uliyoishi na ukataka kutambuliwa kwa hilo bali jitahidi katika muda wowote utakaoishi uache kitu chenye manufaa ambacho katika msiba wako watu watakisimulia.