Posts

Showing posts from April, 2022

KULALAMIKA

Dunia huwa inatupa kile tunachokitaka na tunakizungumzia kila mara katika midomo yetu. katika jamii zetu kulalamika ndiyo utamaduni uliozoeleka, ukienda ofisini watu wanalalamika, kwenye usafiri watu wanalalamika, kwenye nyumba za ibada watu wanalalamika. Hivi ni eneo gani la maisha yako umeona sehemu ambayo watu hawana utamaduni wa kulalamika? Binadamu tumekuwa ni watu ambao tumekosa shukrani, hata tupewe nini hatuwezi kukosa shukrani. Tunajiona hatuna kitu fulani kwa sababu maisha yetu tumeyaweka katika vitu, tunaishi kwa ulinganishi wa vitu na pale tunapojaribu kulinganisha tunajikuta tunaumia na hatuna kitu. Hakuna mtu ambaye amejitosheleza kwa kila kitu, tunatakiwa kushukuru kwa kile ambacho kipo ndani mwetu, tusiangalie tumekosa nini, badala yake tukumbuke tumepata nini, tukiwa tunaangalia vile ambavyo tunavyo maisha ni mazuri sana lakini tukiwa tunaangalia vile ambavyo hatuna maisha yanakuwa siyo mazuri sana. Tunapoteza maana ya maisha yetu pale tunapokuwa tunajilinganisha...

UKUBWA WA HARUSI

Haijalishi ukubwa wa harusi uliyofanya, kitu cha muhimu ni unachokwenda kukijenga baada ya harusi, baada ya watu wote kuondoka na kuwaacha peke yenu mwende nyumbani, mkaanzishe maisha yenu. hiko ndicho cha muhimu na ndicho kinachotakiwa kupewa umakini mkubwa. Sio kwako tu hata kwa taifa. Kwakuwa familia ni kiwanda cha kutengeneza raia wema. Usisahau hilo jua kwamba una kazi kubwa mbele yako, na usichukulie harusi kwa ukubwa usiostahili zaidi ya kile unachoenda kukijenga. "Familia" Harusi na majigambo yake yote sio muhimu kiasi hiko. Harusi ni ya siku moja, lakini unachokwenda kukijenga huenda kikaishi muda, zaidi ya uhai wako. Kwakuwa misingi utakayo wajengea watoto wako ndio misingi hiyo hiyo watakayo wajengea watoto wao. Ubora wa familia yako huenda ukawa pia ubora wa familia zao. Wewe na mke wako mtakapofutika kwenye uso wa dunia, maisha yao duniani yatategemea misingi mliyowajengea. Kwahiyo kuwa makini zingatia haya. Ongoza watoto waliotoka katika tumbo lako vyema n...

TAFAKURI TUNDUIZI

TAFAKURI TUNDUIZI TIBA YA MAENDELEO UTANGULIZI Umewahi kujiuliza kwanini watu hugombana katika mijadala? Kwanini kuna migogoro kati ya nchi na chi, mtu na mtu ama jamii na jamii? Kwanini baadhi ya miradi ya kitaifa haikamiliki ama hukamilika kwa mashaka? Masuala yote hapo juu ni matokeo ya kukosa uwezo wa kufikiri kwa makini, yani, tafakuri tunduizi. Katika kitabu chao The Miniature Guide to Critical Thinking Concepts and Tools, Paul Richard na Linda Elder wanatukumbusha kuwa kila mwanadamu amepewa uwezo wa kufikiri kwakuwa hiki ni kitendo cha asili. Lakini, wanaonya kuwa ili kuwa na fikra makini, ni lazima tujifunze kwakuwa uwezo wetu wa kufikiri una mipaka. Ni vema watoto wakafunzwa tafakuri tunduizi ili kupunguza ubinafsi. Ukosefu wa fikra makini hupelekea mijadala dhaifu, migogoro isiyo na tija na maamuzi dhaifu au hatarishi. TAFAKURI TUNDUIZI NI NINI? Katika mjadala wetu, tutatumia fasili ya Elder na Paul (wametajwa hapo juu). Wao wanaona tafakuri tunduizi ni sanaa ya kuchamb...

MAENDELEO

Maendeleo yote ya binadamu yametokana na gunduzi alizofanya, kwahiyo tunapozungumzia maendeleo ya binadamu hatuwezi kuepuka kuongelea gunduzi alizofanya na ukuaji wa kiakili wa jamii husika. Huu ugunduzi na uzalishaji mali ndio ulikuwa chimbuko la maendeleo na biashara katika jamii nyingi. Jamii zilizozalisha zaidi zilifanya biashara na kupata faida. Waliuza bidhaa walizogundua na kujiongezea mitaji na mahitaji pia ya malighafi yaliongezeka, yaliyowafanya watoke kutoka katika nchi zao kwenda nchi nyingine kuyatafuta, pamoja pia na kutafuta masoko ya bidhaa zao. Kwahiyo pasipo gunduzi maendeleo ya binadamu yangeendelea kuwa duni. Kwahiyo tukizungumza maendeleo tunazungumza ''material things'' na mara nyingi hatumzungumzii binadamu mwenyewe bali vitu alivyofanya na mali anazomiliki. So mahitaji ndio yaliyofanya watu kufikiria kugundua na ndio hapo maendeleo yalipokuja haya tunayoona ya vitu. Mahitaji ya kukabiliana na baridi yaliwafanya watu wagundue moto. Katika kila ...